UONI HAFIFU UNAOWEZA KUREKEBISHWA NA MIWANI/OPERESHENI (SEVERE REFRACTIVE ERRORS)
Baadhi ya udhaifu wa mfumo wa kupitisha taswira ya vitu tunavyoviona kutoka kwenye kioo cha mbele ya jicho mpaka kwenye retina husababisha uoni hafifu ambao hutuletea ugumu katika shughuli zetu za kila siku.
Hali hii ya kushindwa kuona mbali kitaalamu inaitwa (myopia)kushindwa kuona karibu huitwa (hyperopia)
Kwa wale wasioweza kuona mbali na vipimo vyao kuonyesha wanahitaji lensi yenye nguvu ya -6.00 D au zaidi uwezo wao wa kuona huwa ni hafifu hata kufikia upofu.
Wagonjwa hawa wanahitaji kupata vipimo zaidi na kujulikana kama lensi za kuweka machoni,vifaa tiba vya wenye uoni hafifu au operesheni inaweza kuwafaa