Chanzo:
Kwa wagonjwa walio wengi chazo kutofahamika, kwa wachache kuharibika kwa mzunguko wa maji ya jicho kulikosababishwa na magonjwa ya macho/mwili, mara nyingine ugonjwa huwa ni wenye kurithiwa na hasa kwa wenye asili ya Uafrika
Dalili:
Kuona rangi za upinde wa mvua, uoni kuwa wenye ukungu kupata shida kutembea katika njia zenye mashimo, kupanda au kushuka ngazi kwa shida, kupoteza uwezo wa kuona pembeni na maumivu makali ya jicho kwa wagonjwa wachache.
Vigezo vya utambuzi:
Presha ya juu ya jicho kuwa ipo juu ya kiwango cha kawaida ambacho ni (10-21 mmHg) ikiambatana na kunyauka kwa mshipa wa fahamu ya uoni na kusababisha uwezo wa kuona pembeni kuwa mfinyu.
Madhara:
Kunyauka kwa mshipa wa fahamu ya kuonea na mabadiliko haya kama hayatadhibitiwa mapema hupelekea upofu wa kudumu
Kinga:
Hakuna kinga ya kutokuupata ugonjwa huu ila kinga za kuzuia upofu uletwao na ugonjwa huu zipo
Lengo la matibabu:
Kuzuia mgonjwa asifikie upofu wa kudumu
Matokeo ya matibabu:
Matibabu stahiki na kwa wakati hupunguza uwezekano wa mgonjwa kufikia upofu wa kudumu. Tiba zitumikazo ni pamoja na dawa za matone/vidonge za kushusha presha ya jicho, tiba ya mwanga (Laser therapy) na upasuaji. Matokeo ya matibabu yasiyoridhisha husababishwa na mgonjwa kutambulika akiwa amechelewa na madhara ya ugonjwa kuwa tayari ni makubwa, na kutopata tiba sahihi na endelevu.