ATHARI ZA KISUKARI NA SHINIKIZO LA JUU LA DAMU (BP) KATIKA RETINA (PAZIA YA NYUMA YA JICHO)
Dalili:
Kisukari au Shinikizo la juu la damu kutodhibitiwa vya kutosha na kuharibu mishipa midogo ya damu nyuma ya jicho.
Vigezo vya utambuzi:
Mgonjwa wa kisukari/Shinikizo la juu la damu anayefahamika au hata mtu ambaye hakuwa anajijua kuwa na maradhi haya mwenye dalili zilizotajwa hapo juu na kwenye retina yake kukutwa na damu, mafuta au maji yaliyotuama
Madhara:
Kusababisha uoni hafifu na hata kufikia upofu usio tibika (Irrevisisble blindness), kusababisha kupanda presha ya jicho na kuleta maumivu makali kwa wagonjwa watakao chelewa kupata matibabu.
Kinga:
Kwa watu wazima wote kupima sukari, damu na wingi wa mafuta katika damu japo mara moja kwa mwaka, kupunguza uzito wa kupitiliza. Wagonjwa wa Kisukari/Shinikizo la juu la damu kupimwa macho na wataalamu wa macho mara tu wanapogundulika kuwa na maradhi hayo. Wagonjwa wa Kisukari/ Shinikizo la juu la damu kupata tiba muafaka wakati wote
Lengo la matibabu yatolewayo:
Kuzuia madhara zaidi ya Kisukari /BP katika macho na hivyo kupunguza uwezekano wa mgonjwa kufikia upofu wa kudumu.
Matokeo ya matibabu:
Matibabu stahiki na kwa wakati hupunguza uwezekano wa mgonjwa kufikia upofu wa kudumu. Tiba zitumikazo ni pamoja na sindano za ndani ya jicho, tiba ya mwanga (Laser therapy) na upasuaji. Matokeo ya matibabu yasiyoridhisha husababishwa na mgonjwa kuchelewa kutambulika na hivyo kufanya ugonjwa kuwa umeshapevuka mno kuweza kutibika na mgonjwa kumsaidika.