Utangulizi: Lensi ya jicho kupata ukungu na kuzuia mwanga kuingia ndani ya jicho (sababu; uzee, kuumia, magonjwa ya jicho/ ya mwili, maambukizi kwa mtoto wakati wa ujauzito), matumizi ya bidhaa hatarishi na matumizi yasiyo sahihi ya baadhi ya dawa
Dalili: Kufifia uwezo wa kuona mbali/ karibu, kuwepo Uweupe katikati ya mboni ya jicho
Vigezo vya utambuzi: kuwepo kwa mtoto wa jicho anaye sababisha uoni hafifu unao ambatana na kushindwa kutimiza majukumu ya kawaida ya kila siku katika maisha
Madhara: Kusababisha uoni hafifu na hata kufikia upofu, kusababisha kupanda presha ya jicho na kuleta maumivu makali
Kinga: Kutumia vifaa kinga vya macho (protective goggles), matumizi sahihi ya dawa za jamii ya steroids, muhimu; mtoto wa jicho anayetokana na uti uzima hana kinga
Matibabu yatolewayo kwa ugonjwa wa mtoto wa jicho; Operesheni ya mtoto wa jicho
Lengo la matibabu yatolewayo: Kumwezesha mgonjwa kuona vizuri kama ilivyokuwa awali, kwa kutumia miwani kabla watoto wajicho hawajakomaa sana na wakishakomaa kufanyiwa tiba ya upasuaji (kuchunwa, kukwanguliwa, kusafishwa)
Matokeo ya matibabu: Matibabu muafaka na kwa wakati huwezesha mgonjwa kuona vizuri kama zamani, matokeo ya upasuaji yasiyoridhisha husababishwa na mgonjwa kuwa na magonjwa ya macho zaidi ya mtoto wa jicho, teknolojia hafifu iliyotumika, na kutokupata au kuzingatia matibabu sahihi baada ya upasuaji