1. Utangulizi:
yanayoweza kusababisha hali ya upofu kwa wagonjwa walio na umri wa miaka 16 au chini ya hapo. Maradhi kama mtoto wa jicho, presha ya macho, saratani za kwenye macho, maradhi ya kijenetik yaletayo madhara kwenye macho, maambukizi kabla, wakati na baada ya kuzaliwa, ajali za kwenye macho n.k.
2. Dalili; Kufifia uwezo wa kuona mbali/ karibu, mabadiliko ya muonekano wa nje au ndani ya jicho mfano; kupata kengeza, kupatikana uweupe katikati ya mboni ya jicho, kutokwa matongotongo, kifuniko cha juu cha jicho, kuvimba/kuziba jicho n.k
3. Vigezo vya Utambuzi; Mgonjwa mwenye umri wa miaka 16 au chini ya hapo kuwa na dalili ziliotajwa hapo juu.
4. Madhara; Kudumaa kwa kuwa uwezo wa uoni ikiwa maradhi haya yataanza mapema kabla ya umri wa miaka mitano. Baadhi ya maradhi haya hususan lile la saratani ya jicho (Retinoblastoma) ni ugonjwa wa hatari na unaweza kupelekea kifo. Mojawapo ya dalili kubwa za ugonjwa huu ni jicho/macho ya mtoto kupata uweupe kwenye mboni ya jicho hali inayofanana na mtoto wa jicho, na nyingine ni jicho/macho kuanza kuwa na kengeza. Dalili zingine ni jicho kuwa jekundu au kuvimba. Muhimu; yoyote kati ya dalili hizi mara tu zitakapoonekana ni vyema mtoto kupelekwa kwa daktari wa macho haraka kwa uchunguzi. Baadhi ya maradhi ya kuambukiza katika watoto wachanga (Opthalmia neonatorum) ni ya hatari na yanaweza kusababisha jicho kuharibika kabisa.
5. Kinga; Kinga ya kutumia dawa ya
wote mara baada tu ya kuzaliwa hupunguza kwa kiasi kikubwa maambukizi ya macho kwa watoto wachanga (Ophthalmia neonatorum). Kinga zingine ni kama vile chanjo ya surua, matone ya vitamin A nk.
6. Lengo la matibabu; Lengo la matibabu ya maradhi ya macho yanayoleta upofu utotoni hutolewa kwa kuzingatia maradhi husika. Lengo kuu huwa ni kuwezesha uwezo wa mtoto kuona ukuwe katika hali ya kawaida.
7. Matokeo ya matibabu; Mara nyingi tiba ya maradhi ya macho utotoni ni ya muda mrefu,hivyo mzazi/mlezi anashuriwa kufuatilia tiba ya mtoto kikamilifu ili aweze kupata matokeo mazuri.